Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

Power and Duties

Kazi na Mamlaka ya Tume

Kazi za Tume

Kwa mujibu wa vifungu namba 12, 13 na 37 vya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma , kazi na majukumu ya Tume ni pamoja na:

   • Kupokea na kuhifadhi Tamko la Taarifa za Mali na Madeni linalowasilishwa na Kiongozi wa Umma kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;
   • Kupokea tuhuma na taarifa za uvunjwaji wa maadili kutoka kwa wananchi;
   • Kufanya uchunguzi juu ya madai au tuhuma za uvunjwaji wa maadili dhidi ya Kiongozi yeyote wa Umma;
   • Kupokea, kuchunguza na kushughulikia madai yote yanayohusu uvunjwaji wa maadili katika taasisi za umma;
   • Kuchunguza mwenendo wa Kiongozi yeyote wa Umma ambao kwa maoni ya Tume, unapelekea au unachangia uvunjwaji wa maadili chini ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;
   • Kusikiliza na kutoa maamuzi kuhusu madai yoyote ya uvunjwaji wa maadili dhidi ya Kiongozi wa Umma; na
   • Kuelimisha umma juu ya umuhimu wa maadili.

Uwezo wa Tume

   • Kumuagiza ofisa yeyote wa Tume kufanya uchunguzi wa tuhuma yoyote ya uvunjwaji wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Sheria Nam. 4 ya mwaka 2015;
   • Kumtaka kwa maandishi, mtu yeyote au taasisi yoyote kutoa au kuwasilisha taarifa au kujibu maswali au kuwasilisha kumbukumbu au nyaraka zozote zinazohusiana na tuhuma zinazohitaji kufanyiwa uchunguzi; na
   • Kuchunguza Akaunti yoyote ya Benki ambayo Tume inataka kujiridhisha kuhusu hesabu zake, hesabu za hisa, hesabu za manunuzi au nyaraka zozote zinazohusiana na akiba au amana.