Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

Historia

Kuhusu TUME YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA

Hadhi na Historia ya Tume ya Maadili:

Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma ni wakala wa Serikali ambayo imeanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Sheria Nam. 4 ya mwaka 2015. Tume imeanza kufanya kazi mwezi wa Aprili, 2016.

Tume ya Maadili

Tume inaundwa na Mwenyekiti na Makamishna wawili ambao wanateuliwa na Rais wa Zanzibar kwa mujibu wa kifungu cha 5 na 6 cha Sheria ya Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma. Mwenyekiti na Makamishna wanatumikia nafasi zao kwa kipindi cha miaka mitano na wanaweza kuteuliwa tena kwa kipindi chengine.

Sifa:

Kwa mujibu wa kifungu cha 7 cha Sheria, Mtu atakayeteuliwa kuwa Mwenyekiti ni lazima awe ni Mzanzibari mwenye sifa za kuwa Jaji wa Mahkama Kuu, mwenye heshima, ueledi, uaminifu, uadilifu na asiye na tabia au mwenendo wenye kutiliwa shaka. Aidha Makamishna nao wanatakiwa wawe ni wazanzibari wenye sifa za ueledi, uzoefu na uaminifu.

Mtu hatofaa kuteuliwa kuwa Mwenyekiti ikiwa:-

      1. ni mjumbe wa Baraza la Wawakilishi au Mbunge;
      2. (b) ni mtu aliyetangazwa kuwa amefilisika; au
      3. ni mtu aliyetiwa hatiani na Mahakama au chombo chengine chochote cha kinidhamu kwa makosa ya uadilifu au uaminifu.