Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

Ujumbe wa Mwenyekiti

Ujumbe kutoka kwa Mwenyekiti

Welcome to the official website of the Zanzibar Public Leaders’ Ethics Commission (Ethics Commission).  The Ethics Commission is an independent agency of the Zanzibar Revolutionary Government responsible for implementation and enforcement of the Zanzibar Public Leaders’ Code of Ethics Act, No. 4 of 2015 which requires all public leaders to make declaration of their assets and liabilities to the Ethics Commission.

Dhamira ya Tume ya Maadili ni kukuza uadilifu, tabia na mwenendo wenye kufuata maadili kwa Viongozi wa Umma. Dhamira hii itafikiwa kwa kuimarisha uwazi, uwajibikaji, utii na usimamizi wa Sheria pamoja na kujenga uelewa na kutoa elimu kwa umma juu ya umuhimu wa Maadili.

Ni matarajio yangu kuwa, kupitia tovuti hii, itakuwa rahisi kupata taarifa za Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma. Taarifa zinazopatikana kupitia tovuti hii ni pamoja na matakwa ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Nam. 4 ya mwaka 2015 pamoja na taarifa nyengine ambazo zitakupa uelewa mzuri wa masuala ya maadili zikiwemo; Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Nam. 4 ya mwaka 2015, Kanuni na Matangazo ya Kisheria, Fomu ya Tamko la Mali na Madeni, Fomu ya Malalamiko ya Wananchi na ripoti mbalimbali za Tume ya Maadili. Aidha, utaweza kupata taarifa zinazohusiana na Dira, Dhamira, Misingi ya Maadili, Majukumu, Uwezo na Mamlaka pamoja na Muundo wa Tume ya Maadili.

Taarifa zote muhimu zinazohusiana na Tume pamoja na tamko la mali zinapatikana katika ukurasa wa mbele. Napenda kukushajihisha kuipitia tovuti yetu na kuwasiliana nasi kupitia namba +255-24-2235535 kwa huduma na msaada. Wafanyakazi wetu wapo tayari kukusaidia ipasavyo kujibu masuali yanayohusiana na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma pamoja na mambo mengine yanayohusiana na maadili.

Ah’sante, kwa kutembelea tovuti yetu na tunakushukuru kwa kuonesha shauku ya kuifahamu Tume ya Maadili. Tafadhali wasiliana nasi ili tukusaidie au utusaidie kuimarisha huduma zetu.