The Revolutionary Government of Zanzibar

Masheha na Madiwani Wapewa Somo la Maadili ya Uongozi

 

VIONGOZI na Watumishi wa Umma, wametakiwa kufuata  misingi na maadili  ya Umma, ili kuleta maendeleo na kuimarisha utawala bora nchini. Akitoa mafunzo ya Maadili ya Uongozi kwa Masheha na Madiwani wa Wilaya ya Mjini Unguja, huko katika ukumbi wa skuli ya Lumumba Mjini Unguja.
Ofisa Usajili Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma Zanzibar, Abdulatif
Ali, amesema kufuata misingi na maadili ya umma yanapelekea kuwepo uwajibikaji mzuri na uadilifu katika utekelezaji wa majukumu katika jamii
Masheha, Madiwani wapewa somo la maadili ya uongozi Amesema maadilii kwa viongozi na watumishi wa umma hujenga uaminifu na utendaji kazi kiufanisi kwa kuimarisha utawala bora na kuleta maendeleo kwa kukuza
uchumi wa nchi. Ofisa huyo, ameleza lengo la mafunzo hayo ni kuwaweka
viongozi na watumishi wa umma kufuata misingi na maadili umma na kutokuvunja sheria ya maadili ya umma, ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji.
“Mgongano wa maslahi ni miongoni mwa matatizo yanayorejesha nyuma maendeleo ya nchi na kuhakikisha wanafanya majukumu yao bila ya upendeleo kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa na tume hiyo”, amefahamisha Ofisa huyo.
Nae Ofisa Habari wa Tume, Halima Jumbe Said, amewasisitiza viongozi hao
kuyatumia mafunzo ya maadili ya umma, ili kuwa viongozi bora na kuleta maendeleo ya nchi. Amewataka viongozi hao kuzitumia vyema nyadhifa zao
walizopewa katika kuwatunikia wananchi na kuacha tabia ya kujipatia maslahi binafsi kwa lengo la kuleta maendeleo katika jamii. Nao Masheha hao
wameiomba tume ya Maadili kuwapatia viongozi wa umma mwongozo wa Sheria utakaowasaidia katika kutekeleza majukumu kwa uweledi.